Saturday, 7 November 2015

MANCHESTER UNITED YAIUA WEST BROM

 
Jesse Lingard alifunga bao lake la kwanza akiichezea Manchester United huku timu hiyo ya Louis Van Gaal ikiishinda West Bromwich.Winga Lingard mwenye umri wa miaka 22 alifunga bao zuri alipomwangalia kipa wa West Brom na kuuficha mpira ule katika wavu na kuiweka kifua mbele timu hiyo.

JESHI LA YEMEN LAHARIBU MELI YA KIVITA YA SAUDIA


Jeshi la Yemen limetangaza kuwa limelipua meli nyingine ya kivita ya unaoitwa muungano wa nchi za Kiarabu unaoongozwa na Saudi Arabia katika mashambulizi dhidi ya Waislamu wa Yemen.

CCM YANYAKUA VITI 64 MAALUMU,CHADEMA 36


Chama cha CCM kimenyakua idadi kubwa ya viti vya wabunge maalum miongoni mwa vyama vilivyoshiriki katika uchaguzi mkuu uliopita.CCM kimejipatia viti 64, huku CHADEMA kijipatia viti 36 kulingana na tume ya uchaguzi nchini humo.

Chama cha Upinzani CUF nacho kimejipatia viti 10.

WASYRIA WATAKIWA KUFANYA MAZUNGUMZO

Vyama vya siasa nchini Syria vimesema kutumia njia za kisiasa na mazungumzo baina ya Wasyria wenyewe ndilo chaguo pekee la kumaliza mgogoro wa nchi hiyo. Vyama hivyo vimetoa sisitizo hilo katika kikao maalumu kilichofanyika jana Jumamosi mjini Damascus chini ya anuani: "Utatuzi wa kisiasa wa mgogoro wa Syria" na kueleza kwamba kuna ulazima wa kufanyika mazungumzo baina ya Wasyria wenyewe kwa kushirikisha vyama na makundi yote ya nchi hiyo.

MAGUFULI AAGIZWA KUMALIZA MGOGORO ZANZIBAR

 
Marekani imeitaka serikali ya Tanzania kuheshimu maamuzi ya raia wa Zanzibar katika uchaguzi wa urais uliopita.
Akimtumia risala za pongezi rais mpya wa Tanzania John Pombe Magufuli kwa ushindi wake wa uchaguzi mkuu uliopita, waziri wa maswala ya kigeni nchini humo John Kerry amesema kuwa Marekani inaendelea kukerwa na hatua ya kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi huo.